Leo tarehe 3 Novemba 2020 kumefanyika mahafali ya 31 ya kidato cha nne katika shule yetu ya Lwandai inayomilikiwa na Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, ambapo wanafunzi 50 (wa kike 26 na wa kiume 24) wamehitimu. Mgeni rasmi katika mahafali haya alikuwa Mchungaji Peter Bendera (Mkuu wa Dinari ya Kaskazini).
Mahafali haya yalifana sana yakipambwa na vishirikisho mbalimbali toka kwa wahitimu na wanafunzi wengine. Mchungaji Peter Bendera aliwaasa wahitimu
kuendelea kujitahidi kusoma kwa bidii, na kwamba wazingatie maadili mema katika maisha yao. Pia aliwatakia baraka katika mitihani yao inayotazamiwa kuanza Novemba 23-2020. Kulifanyika pia maombezi maalumu kwa wahitimu, kidato cha pili, walimu na wanafunzi wote yaliyoongozwa na wachungaji.