Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 23/05/2021 ametembelea na kuonana na wanafunzi,walimu pamoja na wafanyakazi wa Shule ya Sekondari Lwandai inayo milikiwa na KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa lengo la kuwasalimu.
Amesema amefurahi kuona mazingira ya shule yakiwa katika hali nzuri na rafiki kwa wanafunzi kujifunza huku akiupongeza uongozi wa Shule kwa juhudi wanazoendelea kuzifanya ili kurudisha heshima ya shule ya Lwandai huku akiridhishwa na Idadi ya walimu waliopo.
Awali Baba Askofu Dkt Mbilu alishiriki katika ibada ya Jumapili iliyokuwa na tendo la kuingizwa kazini kwa Mkuu wa jimbo la Kaskazini,Mch Anderson Kipande, Ibada ilifanyika katika kanisa la Mlalo Hoheni.